PEEEEEOPLE'S POOOOOOOWEEEEEER NGUVU YA UMMAAA
Saturday, 2024-04-20
My site
PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Site menu
Our poll
Rate my site
Total of answers: 3
Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
Main » 2012 » May » 11

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), leo anatarajiwa kuanza ziara ya kukijenga chama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kutoka Mbeya, Sugu alisema kuwa anaanza ziara ya kichama ya siku tatu mkoani Ruvuma, ambako atahutubia mikutano ya hadhara.

Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ alisema kuwa leo atafanya mkutano huko Madaba na kesho atakuwa mji mdogo wa Mbinga na Jumapili atamalizia mjini Songea.

"Leo nitaanza ziara ya siku tatu ya kichama mkoani Ruvuma, ambako nitaungana na viongozi wengine wa Chachema mkoani humo, kuhutubia mikutano ya hadhara ili kusaka wananchama wapya kutoka Nyanda za Juu Kusini,” alisema Sugu.

Katika hatua nyingine, Sugu alisema kuwa anashukuru kuona ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katikati ya mji wa Mbeya unaendelea vizuri, jambo linalompa faraja kwamba anatekeleza ahadi zake za kuwaletea maendeleo wakazi wa Mbeya.

Alisema ... Read more »

Views: 2539 | Added by: twangaraha | Date: 2012-05-11 | Comments (0)

MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), amesema kuwa hana nia wala dhamira ya kuchochea na kuhamasisha mgawanyiko katika nchi kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, juu ya maneno anayodaiwa kuyatoa Jumamosi kwenye mkutano wa hadhara wa chama chake wakati wa uzinduzi wa operesheni ‘vua gamba vaa gwanda’ kwenye viwanja vya NMC, Nassari alidai lengo la hotuba yake lilikuwa kuhimiza serikali na jeshi la polisi lishughulikie mauaji ya watu na kudai hakulenga kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake.

"Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa; chama changu siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini wala historia, ningependa ifahamike kuwa sina lengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile kama ambavyo imekuwa ikita ... Read more »

Views: 1315 | Added by: twangaraha | Date: 2012-05-11 | Comments (0)

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetishia kuweka hadharani majina ya mawaziri na wabunge ambao walikuwa tayari kujiunga na chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uenezaji wa chama hicho, John Mnyika, alisema Chama cha Mapinduzi kisitake kuilazimisha CHADEMA iseme ukweli wote juu ya wimbi kubwa la wana CCM, wakiwemo wabunge na mawaziri ambao wanataka kujiunga nayo.

Mnyika akijibu taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, alisema kuwa viongozi wengi wa chama hicho tawala wanajua mchakato mzima uliokuwepo wa wabunge, mawaziri na wana CCM wengine kutaka kuhamia CHADEMA tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 lakini wakaingiliwa.

Mnyika aliwataka viongozi wa CCM waseme kama wako tayari kupokea ukweli mchungu wa viongozi wao walio tayari kukihama chama hicho na kujiunga na upinzani "Wasitulazimishe kusema. Na kama wanataka waseme kama wak ... Read more »

Views: 1528 | Added by: twangaraha | Date: 2012-05-11 | Comments (0)

SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake la mawaziri, mawaziri na manaibu wapya wamesema watahakikisha wanafanya kazi kwa maslahi ya Taifa na Watanzania.

Juzi Rais Kikwete alifanya uteuzi huo kwa kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza lake kwa kuingiza sura 13 mpya huku mawaziri na naibu mawaziri nane wakitupwa nje ya baraza hilo.

Katika mabadiliko hayo, amewapandisha naibu mawaziri wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha mawaziri nane na naibu mawaziri sita, huku mawaziri na naibu mawaziri 22 wakibaki katika wizara zao za awali.

Dk Mgimwa

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, alisema uteuzi huo ni jambo la heshima hivyo ni lazima kujituma na kufanya kazi kwa maslahi ya Watanzania.

Alipoulizwa jinsi atakavyokabiliana na changamoto ndani ya wizara hiyo ikiwa ni pamoja na tuhuma zilizomng ‘oa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Mustapha M ... Read more »
Views: 1288 | Added by: twangaraha | Date: 2012-05-11 | Comments (1)

Lowassa awatuliza wanaCCM wasihamie Chadema
... Read more »
Views: 2079 | Added by: twangaraha | Date: 2012-05-11 | Comments (0)

IKULU imeiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kuwachunguza watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma ambao ndio chanzo cha mawaziri wao kuwajibishwa.

 Hii ni kauli ya kwanza ya Ikulu, tangu Rais Jakaya Kikwete afanye mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri kwa kuwaondoa mawaziri sita ambao wizara zao zilitajwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukabiliwa na kashfa ya ufisadi na matumizi mabaya yafedha za umma.  

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue juzi aliliambia Mwananchi kuwa tuhuma zote ambazo zilibainishwa katika ripoti ya CAG katika maeneo mbalimbali sasa zitachunguzwa na Takukuru pamoja na DCI.  "Tuhuma zote zitapitiwa na vyombo husika (Takukuru na DCI), kitakachofanyika ni kuzipitia tuhuma zote ili kuwatambua wahusika sahihi,” alisema Balozi Sefue.  Alifafanua kwamba uchunguzi huo unafanyika ili ... Read more »
Views: 635 | Added by: twangaraha | Date: 2012-05-11 | Comments (0)

CHADEMA, NCCR MAGEUZI, CUF WAUNGANA KUUPINGA, MADIWANI TARIME WAMKATAA DC

UTEUZI wa wakuu wa wilaya uliotangazwa juzi umezua mjadala baada ya watu wa kada tofauti wakiwemo wasomi, wanasiasa, wanaharakati na wananchi wa kawaida, huku wengine wakidai kwamba ni sehemu ya kulipana fadhili pia mpango maalum wa CCM kupanga safu yake katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Habari kutoka ndani ya CCM zinadai kuwa baadhi ya makada wanautizama uteuzi huo kama moja ya hatua za kuumiza kambi mojawapo ndani ya chama hicho, wakati kikielekea katika uchaguzi wake wa ndani ambao mchakato wake tayari umeanza.

Hata hivyo, wakati wadau hao wakikosoa uteuzi huo, CCM kwa upande wake kimepuuza madai hayo na kuwataka wanaodhani kuna tatizo la kikatiba, kupeleka hoja zao kwenye Tume ya Kukusanya maoni ya Katiba Mpya, ili yafanyiwe kazi.

Katika uteuzi huo, ambao Rais alifanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya zote nchini, wamo waandishi wa habari, wabunge wa viti ... Read more »
Views: 673 | Added by: twangaraha | Date: 2012-05-11 | Comments (0)

Login form
Calendar
«  May 2012  »
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031
NATHASON THE GREAT © 2024