PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Statistics |
Total online: 1 Guests: 1 Users: 0 |
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA
KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
|
Main » 2012 » May » 17 » Mzee Makamba awarushia kombora Nape, Pinda
2:15 AM Mzee Makamba awarushia kombora Nape, Pinda |
ASEMA NAPE ANAIGEUZA CCM MALI YAKE,PINDA YUKO MBALI NA WANANCHI, KINGUNGE PIA ACHARUKA Midraji Ibrahim, Dodoma BAADA
ya ukimya wa muda mrefu, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba
ameibuka katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec) na
kumtuhumu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwamba amekigeuza
chama kuwa mali yake binafsi.
Taarifa kutoka ndani ya kikao
hicho, zimesema kwamba Makamba alisema hatua ya Nape kugeuza chama hicho
kama taasisi yake binafsi ndiyo ambayo imesababisha kikose mwelekeo.
Makamba
licha ya kuelekeza mashambulizi yake kwa Nape, alimrushia pia kombora
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa ana uhusiano mdogo na wananchi.
"Mzee
(Makamba) amesema hivi sasa CCM imekuwa kama jogoo anayepelekwa kwa
mganga, kila anakoelekezwa ndo huko, hali hiyo ndiyo inakikumba CCM hivi
sasa. Amemweleza Nape kuwa amegeuza chama kama mali yake binafsi,
anafanya mambo nje ya utaratibu na anaangaliwa tu.”
Makamba
alidai kuwa badala ya sekretarieti kushughulikia matatizo ya chama,
imekuwa ikihangaika na watu kwa sababu ya kutofautiana nao misimamo na
wakati huo wakijidai kuzika tofauti ili kukiimarisha.
Nape alipoulizwa kuhusu suala hilo alipuuza na kusema: "Si kweli, lakini ninyi andikeni tu maana tumewazoea.”
Alipotakiwa
kueleza kama Kingunge na Makamba walisema nini dhidi yake katika kikao
cha Nec alijibu: "Walikuwapo, lakini hakuna kati yao aliyenitaja hata
kwa jina.”
Nape alitumia muda mwingi kulalamika kuwa taarifa
nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa kutoka ndani ya mkutano huo
uliomalizika jana zimetoka kwa watu aliowataja kuwa wana maslahi nazo
binafsi na kuhoji,” Kwa nini msiwe mnasubiri taarifa rasmi (za chama)
ili habari iwe ya ukweli zaidi?”
Mkongwe mwingine wa chama hicho,
Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye anadaiwa kusikitishwa na vitendo vya
rushwa na ugomvi vinavyoendelea ndani ya chama huku vikiangaliwa na
viongozi kama vile vinakistawisha wakati vinakiporomosha.
Kingunge
alidai kuwa hivi sasa chama hicho kimetawaliwa na matajiri ambao ndiyo
wanaopata nafasi za uongozi na maskini wanawekwa kando.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja aliunga mkono suala la Pinda kuwa
na uhusiano mdogo na wananchi na kwamba, amekuwa mkimya zaidi na
hamsaidii Rais Jakaya Kikwete.
"Yule Mwenyekiti wa Shinyanga,
amemweleza Pinda kuwa ng’ombe wakila mazao mtu wa kwanza kuchapwa viboko
ni mchungaji, halafu mmiliki anatozwa faini baadaye. Hivyo, alitakiwa
kuwajibika kwanza kabla ya mawaziri walioondolewa,” kilidokeza chanzo
chetu.
Mgeja alidai kuwa uwajibishwaji wa mawaziri, haukuzingatia
haki kwa sababu George Mkuchika, Profesa Jumanne Maghembe na Hawa
Ghasia walilalamikiwa, lakini kilichofanywa ni kutoa kafara wengine na
hao kubadilishiwa wizara.
Pia, inadaiwa kuwa Mwenyekiti Kikwete
aliwataka wajumbe kuzika tofauti zao ili kuweka msimamo wa pamoja kwa
ajili ya ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 na kwamba adui namba
moja wa CCM hivi sasa ni Chadema.
Rushwa yakishtua chama
Katibu
wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema Nec imejadili changamoto
zinazokikabili chama kwenye uchaguzi unaoendelea na kubaini kuwa rushwa
imekithiri.
Nape alisema tishio la rushwa ni kubwa na mgombea
atayakayethibitika kujihusisha na vitendo hivyo rushwa ataondolewa mara
moja, huku viongozi na watendaji wakitahadharishwa kuchukuliwa hatua za
nidhamu.
"Kwa kisingizio cha kuwasalimia wajumbe, kuwapa nauli au
kujitambulisha. Mgombea atakayethibitika anazunguka au amezunguka
ataondolewa bila kuchelewa katika orodha ya wagombea,” alisema na
kuongeza:
"Kwa watendaji na viongozi wa chama ngazi zote kuanzia
sasa ni marufuku kuwatembeza ndani ya maeneo yao, kwa nia ya
kuwatambulisha kwa wapiga kura. Mtendaji au kiongozi atakayebainika
anakiuka agizo hili, atachukuliwa hatua za nidhamu mara moja.”
Pia,
Nape alisema kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji na viongozi wa
chama ngazi zote kuwaitia wagombea, wajumbe wa mikutano ya uchaguzi kwa
lengo lolote, kwani vikao vya aina hiyo havimo katika katiba.
Alisema
vikao vya aina hiyo ni haramu na vinapalilia rushwa na kuongeza kwamba
wanachama wa CCM wanatakiwa kupiga vita rushwa na kutoa taarifa ya
vitendo hivyo katika ofisi za chama na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru).
Aliitaka Takukuru kutomuonea aibu au kumuogopa mtu anayejihusisha na vitendo vya rushwa badala yake wamchukulie hatua.
Mishahara na chakula
Kuhusu
mishahara ya watumishi wa umma na mfumuko wa bei ya chakula, Nape
alisema Nec imeagiza Serikali kuhimiza waajiri kupandisha mishahara na
malipo mengine kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha.
Alisema
gharama za maisha zimepanda na mishahara inayolipwa haiendani na hali
halisi. Alisema nayo Serikali inatakiwa nayo kupandisha mishahara kwa
watumishi wake.
"Serikali idhibiti malipo ya huduma ya ndani kwa
kutumia fedha za kigeni, hasa Dola ya Marekani. Pia, iongeze udhibiti wa
maduka na hoteli zinazofanya biashara ya fedha za kigeni ili kuondoa
hujuma kwa uchumi wa nchi inayofanywa kutokana na uhuru uliokithiri
katika biashara hii,” alisema.
Nape alisema Serikali inatakiwa
kuweka jitihada zaidi za kudhibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na
upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi za nyumba na usafiri.
Alisema Nec imeagiza Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na kati za kukabiliana na tatizo la mfumuko wa bei.
"CCM
inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka na muda mfupi ikiwamo
kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) katika sukari,” alisema Nape.
Pia, Nape alisema
wameagiza Serikali kupitia upya utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea
ili upanuliwe kunufaisha wakulima wengi.
Alisema Nec imeitaka
Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa
kuhifadhi chakula nchini, hasa kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Nafaka ya
Taifa (NFRA), ikiwamo kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula maeneo
ya uzalishaji na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ununuzi wa mazao hayo.
"Wakati
wa uhaba wa vyakula maeneo ya mijini, kasi ya kupeleka chakula maeneo
hayo iongezwe na utaratibu mzuri zaidi wa usambazaji chakula utumike ili
walaji na siyo wasafirishaji na wasindikaji, wanufaike,” alisema.source mwananchi
|
Views: 1345 |
Added by: twangaraha
| Rating: 0.0/0 |
|
|
|