PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Statistics |
Total online: 1 Guests: 1 Users: 0 |
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA
KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
|
Main » 2012 » May » 22
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemaliza uchaguzi katika ngazi ya mashina na
matawi huku kikikabiliwa na tatizo la kupata wagombea nafasi ya
mabalozi wa nyumba kumi katika maeneo mbalimbali nchini.Uchunguzi wa
gazeti hili katika mikoa mbalimbali, umebaini kuwa makada wengi wa CCM
walikwepa kugombea nafasi hiyo jambo lililofanya walazimishane na kuleta
wakati mgumu kupata warithi. Kwa mujibu wa Katiba ya CCM,
mabalozi au wajumbe wa shina ndio ngazi ya kwanza ya uongozi ndani ya
chama hicho pia ni kiungo muhimu kati ya chama na wananchi katika maeneo
wanayoishi. Mbali ya majukumu mengine, mabalozi wa nyumba kumi
wamekuwa wahamasishaji wakuu wa chama katika maeneo yao, kuhakikisha
wanachama wanajiandikisha kwenda kupiga kura pia kujua idadi yao kwenye
eneo husika. Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Augustino
Mbogo, amekiri kuwa kazi ya kuchagua mabalozi wa nyumba kumi iliingia
dosari na kufanya baadhi ya watu kususa. Hata hivyo, aliwarushia
lawama
...
Read more »
Views:
14511
|
Added by:
twangaraha
|
Date:
2012-05-22
|
|
SAKATA la Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda kutangaza nia ya
kuwania urais ndani ya Kikao cha Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, sasa
linaitikisa Chadema baada ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la
chama hicho (Bavicha), Joliana Shonza kupingana hadharani na bosi wake,
John Heche. Wakati Heche akiwa tayari ametoa tamko kumshambulia
Shibuda akisema chama hicho hakitaruhusu mgombea wake urais atangaze
nia kwenye vikao vya CCM, Shonza ameibuka na kusema tamko hilo la bosi
wake siyo la Bavicha ila ni lake binafsi. Jana, Shonza akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam, alilikana tamko la Heche wiki
iliyoipita akisema hakuna kikao ambacho baraza hilo lilikaa na kutoa
kauli moja kumjadili Shibuda. Hii ni mara ya tatu kwa Shibuda
kusababisha mgongano ndani ya Chadema. Aliwahi kupinga msimamo wa
kutotambua matokeo ya urais wa Jakaya Kikwete na badala yake, alishiriki
tafrija Ikulu ndogo Chamwino, baada ya mkuu huyo wa nchi kuzindua Bunge
la 10 n
...
Read more »
Views:
4080
|
Added by:
twangaraha
|
Date:
2012-05-22
|
|
KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya
yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri
wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo
hao wanamiliki mali na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi. Maofisa
saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar
es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi. Tuhuma
hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za
ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa kuanza kazi
juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo
itaanza rasmi kazi zake leo. Habari za uhakika kutoka ndani ya
Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja
wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo
mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki
akaunti ya fedha za kigeni. Kigogo huyo anahusishwa pia na mtan
...
Read more »
Views:
8328
|
Added by:
twangaraha
|
Date:
2012-05-22
|
| |
|
|
|