PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Statistics |
Total online: 1 Guests: 1 Users: 0 |
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA
KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
|
Main » 2012 » May » 11
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), leo anatarajiwa kuanza ziara ya kukijenga chama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kutoka Mbeya, Sugu
alisema kuwa anaanza ziara ya kichama ya siku tatu mkoani Ruvuma,
ambako atahutubia mikutano ya hadhara.
Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ alisema kuwa leo atafanya mkutano huko
Madaba na kesho atakuwa mji mdogo wa Mbinga na Jumapili atamalizia mjini
Songea.
"Leo nitaanza ziara ya siku tatu ya kichama mkoani Ruvuma, ambako
nitaungana na viongozi wengine wa Chachema mkoani humo, kuhutubia
mikutano ya hadhara ili kusaka wananchama wapya kutoka Nyanda za Juu
Kusini,” alisema Sugu.
Katika hatua nyingine, Sugu alisema kuwa anashukuru kuona ujenzi wa
barabara kwa kiwango cha lami katikati ya mji wa Mbeya unaendelea
vizuri, jambo linalompa faraja kwamba anatekeleza ahadi zake za
kuwaletea maendeleo wakazi wa Mbeya.
Alisema
...
Read more »
Views: 2402 |
Added by: twangaraha |
Date: 2012-05-11
|
|
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), amesema kuwa
hana nia wala dhamira ya kuchochea na kuhamasisha mgawanyiko katika nchi
kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, juu ya maneno anayodaiwa
kuyatoa Jumamosi kwenye mkutano wa hadhara wa chama chake wakati wa
uzinduzi wa operesheni ‘vua gamba vaa gwanda’ kwenye viwanja vya NMC,
Nassari alidai lengo la hotuba yake lilikuwa kuhimiza serikali na jeshi
la polisi lishughulikie mauaji ya watu na kudai hakulenga kuchochea
vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake.
"Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa;
chama changu siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa
Watanzania wote kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila
kujali ukanda, udini wala historia, ningependa ifahamike kuwa sina lengo
wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile kama ambavyo
imekuwa ikita
...
Read more »
Views: 1254 |
Added by: twangaraha |
Date: 2012-05-11
|
|
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetishia kuweka
hadharani majina ya mawaziri na wabunge ambao walikuwa tayari kujiunga
na chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Uenezaji wa chama hicho, John Mnyika, alisema Chama cha
Mapinduzi kisitake kuilazimisha CHADEMA iseme ukweli wote juu ya wimbi
kubwa la wana CCM, wakiwemo wabunge na mawaziri ambao wanataka kujiunga
nayo.
Mnyika akijibu taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Uenezi na
Itikadi, Nape Nnauye, alisema kuwa viongozi wengi wa chama hicho tawala
wanajua mchakato mzima uliokuwepo wa wabunge, mawaziri na wana CCM
wengine kutaka kuhamia CHADEMA tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010
lakini wakaingiliwa.
Mnyika aliwataka viongozi wa CCM waseme kama wako tayari kupokea
ukweli mchungu wa viongozi wao walio tayari kukihama chama hicho na
kujiunga na upinzani
"Wasitulazimishe kusema. Na kama wanataka waseme kama wak
...
Read more »
Views: 1315 |
Added by: twangaraha |
Date: 2012-05-11
|
|
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko makubwa katika
Baraza lake la mawaziri, mawaziri na manaibu wapya wamesema
watahakikisha wanafanya kazi kwa maslahi ya Taifa na Watanzania. Juzi
Rais Kikwete alifanya uteuzi huo kwa kufanya mabadiliko makubwa ya
Baraza lake kwa kuingiza sura 13 mpya huku mawaziri na naibu mawaziri
nane wakitupwa nje ya baraza hilo. Katika mabadiliko hayo,
amewapandisha naibu mawaziri wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha
mawaziri nane na naibu mawaziri sita, huku mawaziri na naibu mawaziri 22
wakibaki katika wizara zao za awali. Dk Mgimwa Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk
William Mgimwa, alisema uteuzi huo ni jambo la heshima hivyo ni lazima
kujituma na kufanya kazi kwa maslahi ya Watanzania. Alipoulizwa
jinsi atakavyokabiliana na changamoto ndani ya wizara hiyo ikiwa ni
pamoja na tuhuma zilizomng ‘oa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Mustapha
M
...
Read more »
Views: 1196 |
Added by: twangaraha |
Date: 2012-05-11
|
|
Lowassa awatuliza wanaCCM wasihamie Chadema |
|
...
Read more »
Views: 2015 |
Added by: twangaraha |
Date: 2012-05-11
|
|
IKULU imeiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na
Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kuwachunguza
watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma ambao ndio chanzo
cha mawaziri wao kuwajibishwa. Hii ni kauli ya kwanza ya Ikulu,
tangu Rais Jakaya Kikwete afanye mabadiliko katika Baraza lake la
Mawaziri kwa kuwaondoa mawaziri sita ambao wizara zao zilitajwa kwenye
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kukabiliwa na kashfa ya ufisadi na matumizi mabaya yafedha za umma. Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue juzi aliliambia Mwananchi kuwa
tuhuma zote ambazo zilibainishwa katika ripoti ya CAG katika maeneo
mbalimbali sasa zitachunguzwa na Takukuru pamoja na DCI. "Tuhuma zote
zitapitiwa na vyombo husika (Takukuru na DCI), kitakachofanyika ni
kuzipitia tuhuma zote ili kuwatambua wahusika sahihi,” alisema Balozi
Sefue. Alifafanua kwamba uchunguzi huo unafanyika ili
...
Read more »
Views: 589 |
Added by: twangaraha |
Date: 2012-05-11
|
|
CHADEMA, NCCR MAGEUZI, CUF WAUNGANA KUUPINGA, MADIWANI TARIME WAMKATAA DC UTEUZI
wa wakuu wa wilaya uliotangazwa juzi umezua mjadala baada ya watu wa
kada tofauti wakiwemo wasomi, wanasiasa, wanaharakati na wananchi wa
kawaida, huku wengine wakidai kwamba ni sehemu ya kulipana fadhili pia
mpango maalum wa CCM kupanga safu yake katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015. Habari
kutoka ndani ya CCM zinadai kuwa baadhi ya makada wanautizama uteuzi
huo kama moja ya hatua za kuumiza kambi mojawapo ndani ya chama hicho,
wakati kikielekea katika uchaguzi wake wa ndani ambao mchakato wake
tayari umeanza. Hata hivyo, wakati wadau hao wakikosoa uteuzi
huo, CCM kwa upande wake kimepuuza madai hayo na kuwataka wanaodhani
kuna tatizo la kikatiba, kupeleka hoja zao kwenye Tume ya Kukusanya
maoni ya Katiba Mpya, ili yafanyiwe kazi. Katika uteuzi huo,
ambao Rais alifanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya zote nchini, wamo
waandishi wa habari, wabunge wa viti
...
Read more »
Views: 630 |
Added by: twangaraha |
Date: 2012-05-11
|
|
|
|
|
|