PEEEEEOPLE'S POOOOOOOWEEEEEER NGUVU YA UMMAAA
Tuesday, 2022-11-29
My site
PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Site menu
Our poll
Rate my site
Total of answers: 3
Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
Main » 2012 » May » 11 » CHADEMA yatishia kuiumbua CCM
10:48 AM
CHADEMA yatishia kuiumbua CCM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetishia kuweka hadharani majina ya mawaziri na wabunge ambao walikuwa tayari kujiunga na chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uenezaji wa chama hicho, John Mnyika, alisema Chama cha Mapinduzi kisitake kuilazimisha CHADEMA iseme ukweli wote juu ya wimbi kubwa la wana CCM, wakiwemo wabunge na mawaziri ambao wanataka kujiunga nayo.

Mnyika akijibu taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, alisema kuwa viongozi wengi wa chama hicho tawala wanajua mchakato mzima uliokuwepo wa wabunge, mawaziri na wana CCM wengine kutaka kuhamia CHADEMA tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 lakini wakaingiliwa.

Mnyika aliwataka viongozi wa CCM waseme kama wako tayari kupokea ukweli mchungu wa viongozi wao walio tayari kukihama chama hicho na kujiunga na upinzani "Wasitulazimishe kusema. Na kama wanataka waseme kama wako tayari, tufungue boksi, ikibidi hata nitaje majina ya watu na kwa nini baadaye walishindwa kujiunga,” alisema Mnyika.

Mnyika alisema imekuwa ni kawaida ya CCM kukanusha kila kitu, na kumlinganisha Nape na aliyekuwa Waziri wa Habari wa Iraq chini ya utawala wa Saddam Hussein ambaye alikanusha kila kitu, huku akijua majeshi ya Marekani yalikuwa yamewazidi nguvu.

"Sisi hatuwashangai wao kukanusha maana hata wakati waliokuwa madiwani wao wanahama kutoka CCM kuja CHADEMA walikanusha hivihivi, lakini leo yako wapi, madiwani kuanzia Arusha mpaka Mwanza huko wamehamia CHADEMA, hivyo hata hili la wabunge na mawaziri atakanusha sana lakini si atulie asubiri aone,” amesema Mnyika.

Taarifa ya CCM iliyotolewa jana imekanusha madai yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, ambaye mwishoni mwa wiki jana alitangaza katika mkutano mkubwa wa hadhara jijini Arusha kuwa wabunge 70 na mawaziri kadhaa walikuwa tayari kujiunga na chama hicho cha upinzani.

Nape alidai kuwa maneno hayo ya Mbowe ni uongo kwa vile hakuna waziri au mbunge ambaye yuko tayari kuondoka ndani ya CCM na kwamba yametolewa kwa lengo la kujipatia umaarufu wa bure.

Hoja ya mauaji

Akizungumzia tamko la CCM lililotolewa jana kukanusha tuhuma za kuhusika na mauaji, Mnyika alikishambulia vikali chama tawala akidai kimeshindwa, Nape anaficha ukweli juu ya kuhusika kwa baadhi ya viongozi wake na mauaji hayo.

"Kama angetafakari kabla ya kusema angejua kuwa mpaka sasa viongozi wa serikali wanaotokana na CCM wako chini ya ulinzi wa polisi kuhusiana na mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River. Lakini pia viongozi na wanachama wa CCM wametajwa kwa majina kuhusika katika tukio la wabunge wa CHADEMA kukatwa mapanga huko Mwanza. Na mpaka sasa wako chini ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi Mwanza,” alisema Mnyika.

Aliongeza kuwa kuna majina ya viongozi wa CCM waliotajwa kuhusika katika vitendo vya mauaji na vingine vya utekaji kwa wanachama na makada wa CHADEMA katika maeneo mbalimbali mathalani wakati wa uchaguzi mdogo wa Kiteto, Busanda, Biharamulo na kwingine.

Mnyika aliongeza kuwa kama kweli CCM inataka kuonyesha kuwa ina uchungu na inakerwa na wimbi la mauaji ya kisiasa yanayoendelea nchini, basi walizungumze suala hilo katika vikao vyao kuielekeza serikali kutumia sheria ya Inquest Act, sura ya 24 ya sheria za Tanzania ambayo inaitaka serikali kuchunguza vifo vyenye utata.

Views: 1300 | Added by: twangaraha | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *:
Login form
Calendar
«  May 2012  »
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031
NATHASON THE GREAT © 2022