PEEEEEOPLE'S POOOOOOOWEEEEEER NGUVU YA UMMAAA
Wednesday, 2023-02-01
My site
PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Site menu
Our poll
Rate my site
Total of answers: 3
Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
Main » 2012 » May » 11 » Ikulu yaagiza uchunguzi watendaji wizarani, taasisi
10:31 AM
Ikulu yaagiza uchunguzi watendaji wizarani, taasisi
IKULU imeiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kuwachunguza watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma ambao ndio chanzo cha mawaziri wao kuwajibishwa.

 Hii ni kauli ya kwanza ya Ikulu, tangu Rais Jakaya Kikwete afanye mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri kwa kuwaondoa mawaziri sita ambao wizara zao zilitajwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukabiliwa na kashfa ya ufisadi na matumizi mabaya yafedha za umma.  

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue juzi aliliambia Mwananchi kuwa tuhuma zote ambazo zilibainishwa katika ripoti ya CAG katika maeneo mbalimbali sasa zitachunguzwa na Takukuru pamoja na DCI.  "Tuhuma zote zitapitiwa na vyombo husika (Takukuru na DCI), kitakachofanyika ni kuzipitia tuhuma zote ili kuwatambua wahusika sahihi,” alisema Balozi Sefue.  Alifafanua kwamba uchunguzi huo unafanyika ili kuhakikisha kuwa uamuzi utakaotolewa haumuonei mtendaji yoyote. "Tutachunguza na watakaobainika watakachukuliwa hatua za kinidhamu au kufikishwa mahakamani,”alisema Sefue na kuongeza:

"Baada ya Takukuru na DCI kumaliza kazi yao taarifa watakazozitoa zitakwenda kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka), ili kuona kama jambo lililobainika linaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu au kupelekwa mahakamani.”  Balozi Sefue alisisitiza kwamba inafanyika hivyo ili, kuhakikisha hakuna mtendaji yoyote atakayeonewa na pia hawataki mwenye makosa aponyoke.  Aliwataka watumishi na watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma kufanya kazi kwa kukumbuka mambo mawili,  ambayo ni kutambua kuwa wameajiriwa kwa ajili ya Watanzania na kuzingatia maadili ya kazi.  

"Wakitekeleza hayo mawili mambo yanakuwa mazuri zaidi…, mtumishi anatakiwa kutambua kuwa kaajiriwa na wananchi hivyo anatakiwa kujituma na kuzingatia maadili ya kazi,” alisisitiza  Balozi Sefue.  Hata hivyo, imewatoa hofu watendaji wote nchini kwa kuwataka kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kukumbuka kuwa wapo kazini kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania na si vinginevyo.  

Asifia uwazi  Balozi Sefue alisema  sio kweli kuwa hivi sasa vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma vimeongezeka bali hali hiyo inaonekana zaidi kwa sasa kwa kuwa Serikali imekuwa ikifanya mambo yake kwa uwazi mkubwa.  "Hivi sasa ripoti mbalimbali zinawekwa wazi bungeni na wabunge wanachangia, ripoti haziwekwi tena kabatini na hiyo ndio sababu, sio kweli kuwa matukio ya ubadhirifu yameongezeka kwa sasa,” alifafanua Balozi Sefue.  Kauli ya balozi Sefue inakuja wakati tayari CAG , Ludovick Utouh amewaonya mawaziri wapya na watendaji serikalini kwamba ripoti zake hivi sasa zina nguvu za kusimamia uwajibikaji hivyo, wanapaswa kusimamia vema wizara zao kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma.

 Utouh alisema mawaziri wanapaswa kufahamu kuanzia sasa hadi mwaka 2015 zitatoka ripoti nyingine tatu, hivyo ni vyema wakachukua tahadhari kama wasimamizi wakuu wa shughuli za wizara.

 Utouh alisema kilichotokea bungeni na hadi kufikia mawaziri kuwajibishwa, imethibitisha kuwa sasa kutakuwa na uwajibikaji mkubwa utakaosababishwa na ripoti zake kama watendaji wasipofuata taratibu za Serikali.  Wakati akitangaza mabadiliko ya mawziri, Rais Kikwete alisema  baada ya mawaziri kuwajibika kisiasa, wanaofuta ni watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma ambao ndiyo chanzo cha mawaziri hao kujiuzulu.  

Alisema mawaziri wamekuwa wakijiuzulu hata kwa makosa ambayo si yao na kwamba hivi sasa Serikali itaanza kuchukua hatua kwa watendaji wakiwamo makatibu wakuu, wakurugenzi wa wizara, watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za umma pamoja na bodi za mashirika husika.

Mawaziri waliowajibishwa kutokana na matokeo ya ripoti ya CAG ni  William Ngeleja (Nishati na Madini), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), Omar Nundu (Uchukuzi), Mustafa Mkulo (Fedha), Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii) na Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara). Naibu Mawaziri waliokubwa pia na panga hilo ni Dk Lucy Nkya, (Afya) na Athuman Mfutakamba (Uchukuzi).
Views: 584 | Added by: twangaraha | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *:
Login form
Calendar
«  May 2012  »
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031
NATHASON THE GREAT © 2023