PEEEEEOPLE'S POOOOOOOWEEEEEER NGUVU YA UMMAAA
Thursday, 2024-03-28
My site
PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Site menu
Our poll
Rate my site
Total of answers: 3
Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
Main » 2012 » May » 4 » Magufuli: Sijampa Mkulo siku saba
4:56 PM
Magufuli: Sijampa Mkulo siku saba






Magufuli: Sijampa Mkulo siku saba






WAZIRI wa Ujenzi, John Magufuli, amesema hajatoa siku saba kwa Waziri Mustafa Mkulo kama alivyonukuliwa na gazeti la Tanzania daima jana, akidai kutokuwa na mamlaka hayo.
Akizungumza na mwandishi wa Tanzania daima kwa njia ya simu, Magufuli alisema hawezi kutoa amri na agizo la aina hiyo kwa kuwa hana nguvu za aina hiyo kisheria, badala yake alisema amelipa siku saba Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambalo linatakiwa kuhakikisha limeondoa nguzo ndani ya muda huo vinginevyo wataziondoa kwa nguvu.
Tanzania Daima jana liliandika pamoja na matamshi mengine, kuwa Magufuli alikuwa amempa Waziri Mkulo siku saba kuhakikisha kuwa ameruhusu kuondolewa kwa vifaa vya ujenzi bandarini vilivyozuiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) vinginevyo angemshtaki kwa Rais Kikwete.
"Nimekaa serikalini kwa muda wa miaka 18 sasa, nafahamu taratibu za kazi, siamini katika kutishana,” alisema.
Hata hivyo, waziri huyo akakiri kutishia kumshtaki waziri mwenzake kwa Rais Jakaya Kikwete ikiwa kampuni hiyo itacheleweshewa vifaa vyake na hivyo kurudisha nyuma kasi ya ujenzi wa barabara hizo.
Juzi Waziri Magufuli alifanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi, eneo la Ubungo, ambapo alipokea taarifa ya kukwama kwa vifaa vya kampuni ya ujenzi kutoka Ujerumani ya Strabag, bandarini jijini Dar es Salaam, kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha.
"Hili ni agizo la Rais mwenyewe kuhusu upanuzi wa barabara hizi ili foleni ziishe, na waziri analifahamu hilo, nitaongea naye kama akishindwa basi nitamchongea kwa Rais na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nitaongea nayo,” alisema.
Kwa upande wake, Waziri Mkulo alikana kujua chochote kuhusiana na suala zima la kampuni hiyo, na kutaka mambo hayo aulizwe katibu mkuu wa wizara hiyo. Aidha alieleza kushangazwa na kauli hiyo akidai kuwa kama lipo tatizo zipo kanuni na taratibu za kufuatwa na sio kuendesha mambo kupitia magazetini.


Views: 621 | Added by: twangaraha | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *:
Login form
Calendar
«  May 2012  »
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031
NATHASON THE GREAT © 2024