PEEEEEOPLE'S POOOOOOOWEEEEEER NGUVU YA UMMAAA
Tuesday, 2022-11-29
My site
PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Site menu
Our poll
Rate my site
Total of answers: 3
Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
Main » 2012 » May » 13 » mambo yaenda vibaya,ikulu yapingwa
11:31 AM
mambo yaenda vibaya,ikulu yapingwa
WANAHARAKATI nchini wamepinga   mpango wa Ikulu wa kutaka kuwapo na uchunguzi wa watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma wanaotuhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma kwa kigezo kwamba ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inatosha kuwafikisha mahakamani.

Kauli hiyo imekuja baada ya juzi Ikulu  kuagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwachunguza watendaji hao na kwamba uchunguzi huo kwa kile walichoeleza ni ili kutomuonea mtu wala kukandamiza wakati wa kuchukua hatua.

Wakichangia maoni katika mada ya hali ya uwajibikaji nchini iliyotolewa kwenye Semina ya Maendeleo na Jinsia (GDSS), iliyofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam walisema , tuhuma zilizowaondoa kwenye nafasi zao ni za kushindwa kuwajibika na si za rushwa.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia katika mtandao huo, Diana Mwiru alisema kwa sasa hakuna haja ya kufanya uchunguzi kwa kuwa ripoti ya CAG na zile za kamati tatu za Bunge zinaonyesha wazi namna wahusika walivyohusika katika tuhuma hizo.

"Tuhuma zinazowahusu mawaziri zinatokana na wao kushindwa kuwajibika na kulisababishia hasara taifa, … ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali (CAG) na ripoti za kamati tatu za Bunge zote  ziko wazi na wote tumeona hasara iliyotokea ,hoja yangu ni kwamba tunachunguza nini tena? alihoji Mwiru na kuongeza:

"Kinachotakiwa kwa sasa ni  wahusika kufikisha mahakamani kujibu tuhuma, unafanyika uchunguzi mwingine wa nini, hawa wanatufanya sisi hatujui kitu, kazi ya Takukuru ni kuchunguza rushwa swali ni je tuhuma hizo ni za rushwa? alihoji Mwiru.

Mwiru alisisitiza kuwa chunguzi zilizofanywa zinatosha na sasa Watanzania wanataka kuona watuhumiwa wakifikishwa kwenye mhimili mwingine unaotafsiri sheria (Mahakama) ili kuona haki inatendeka.


Mawaziri waliondolewa katika nafasi zao walitajwa katika ripoti ya CAG, na pia ripoti za kamati za kudumu za Bunge zilizowasilishwa kwenye vikao vya Bunge lilifanyika hivi karibuni mkoani Dodoma.

Kamati hizo ni ile ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (POAC) ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mwenyekiti wake , James Lembeli zilionyesha namna mawaziri walivyoshindwa kuwajibika na kusababishia taifa hasara kubwa.

Ripoti za kamati hizo bungeni ziliibua tuhuma za upotevu wa fedha huku zikiwataja baadhi ya mawaziri kushindwa kuwajibika hali iliyomsukuma Mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe kuitisha hoja ya kukusanya saini za kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Akitoa mada katika washa hiyo, Amina Uddy mwanaharakati kutoka ForDIA, alisema hali ya uwajibikaji nchini imeshuka  kwa kiwango kikubwa hali inayowafanya viongozi washindwe kujali na kusimamia rasilimali za umma.
Views: 1341 | Added by: twangaraha | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *:
Login form
Calendar
«  May 2012  »
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031
NATHASON THE GREAT © 2022