PEEEEEOPLE'S POOOOOOOWEEEEEER NGUVU YA UMMAAA
Wednesday, 2023-02-01
My site
PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Site menu
Our poll
Rate my site
Total of answers: 3
Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
Main » 2012 » May » 8 » Nasari sasa kwenye mikono ya dora
3:53 AM
Nasari sasa kwenye mikono ya dora

JESHI la polisi nchini linawashikilia viongozi na wanachama watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku likimpa muda mpaka jana saa 12 jioni mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kujisalimisha vinginevyo wataendesha msako mkali wa kumkata popote alipo.

Nassari na viongozi waliokwishakamatwa wanatuhumiwa kutoa maneno kuwa Ridhiwani Kikwete anao marafiki wa kike anaowatambulisha kwa baba yake Rais Jakaya Kikwete ambaye huwateua kushika nyadhifa mbalimbali kutokana na ushawishi wake.

Naibu Kamishna wa Polisi, Isaya Mngulu, ambaye ni mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini kitengo cha upelelezi (CID) makao makuu ya jeshi hilo aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa kauli hizo zilitolewa kwenye mkutano wao wa Operesheni Vua Gamba Vaa Gwanda walioufanya Jumamosi iliyopita kwenye viwanja vya NMC.

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (BAVICHA), John Heche, Katibu Mwenezi wa CHADEMA Arusha Mjini, Emanuel Kombe na Ally Bananga ambaye alikabidhiwa rasmi kadi ya CHADEMA kwenye mkutano huo akitokea CCM alikokuwa akishika nyadhifa mbalimbali za uongozi.

"Maneno yaliyotamkwa ni yale waliyosema endapo jeshi la polisi litakuwa halijakamata mtu yeyote kuhusiana na mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River wilayani Arumeru, basi rais asikanyage Arusha na wataweka mipaka mikoa ya kanda ya kaskazini na baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa, tena mmoja akijitangaza kuwa rais na mwingine kuwa waziri mkuu,” alisema Mngulu.

Alisema kuwa walimtaarifu Nassari tokea siku ya Jumamosi kuwa wanamhitaji kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano lakini hakutokea ambapo amezima simu zake zote za kiganjani hali iliyomlazimu kumuachia ujumbe wa maneno kwenye moja ya simu zake akijulishwa hilo lakini mpaka jana majira ya saa tisa alasiri hakuwa amefika kituoni hapo.

"Ajisalimishe mwenyewe vinginevyo tutamuadhiri hata huo uheshimiwa wake hatutaujali, Bunge la bajeti linaanza Juni 12 ataendelea kujificha mpaka lini, leo tunatangaza msako kama mpaka saa 12 hajajitokeza tutamsaka mpaka tumtoe huko aliko,” alisema.

Hata hivyo alisema kuwa viongozi hao wakimaliza kuhojiwa wataachiwa lakini taarifa toka kwa watu wa karibu na watuhumiwa hao watatu zilidai kuwa walishamaliza kuhojiwa lakini polisi ilikataa kuwaruhusu kuondoka mpaka hapo mbunge huyo wa Arumeru Mashariki atakapojisalimisha kituoni hapo.

Watuhumiwa wa mauaji wakamatwa

Wakati huohuo jeshi la polisi limewakamata wenyeviti wawili wa vitongoji wa CCM, Dausi Mkumba (Kisambaramajengo), Mathias Nathan( Magadini) pamoja na Katibu wa CHADEMA Kata Usa River Said Mkwela kwa tuhuma za kuhusiana na mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kata hiyo Msafiri Mbwambo aliyeuawa kwa kukatwa shingo na kitu chenye ncha kali usiku wa April 27, mwaka huu.

Mngulu alisema katika uchunguzi wao walibaini kuwa marehemu alikuwa na mzozo na baadhi ya wenyeviti wa vitongozi kutokana na kuwa mstari wa mbele katika kufuatilia taarifa za mapato na matumizi ya miradi mbalimbali ndani ya kata hiyo.

Mngulu alisema kuwa pia marehemu Msafiri alikuwa maarufu sana hivyo kuwa tishio kubwa kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa hali iliyowafanya kumchukia na hatimaye kupanga njama za kumuua ambapo alisema wengine watano wanaendelea kuwahoji.

Akizungumzia matukio mengine ya mauaji yaliyotokea wilayani Arumeru, Mngulu alisema watuhumiwa watatu Godlove Manang’ (26), Antony Kiungai (23) na Judica Kitomary (26) waliwahoji kuhusiana na tukio la kuvamia shamba la Mito Miwili Aprili 28, mwaka huu, ambapo Noel Mangang’ aliuawa na walinzi wa shamba hilo.

Alisema katika tukio hilo wakazi zaidi ya 20 wa Sing’isi wanadaiwa kuvamia shamba hilo na kuvunja stoo wakaiba mbolea, mbegu mbalimbali za mazao kisha wakachoma matrekta na jenereta ambapo thamani ya vitu hivyo inakadiriwa kufikia sh milioni 222.8 ambapo watu hao wamefikishwa mahakamani jana kwa kosa la kuharibu mali.


Views: 567 | Added by: twangaraha | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *:
Login form
Calendar
«  May 2012  »
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031
NATHASON THE GREAT © 2023