PEEEEEOPLE'S POOOOOOOWEEEEEER NGUVU YA UMMAAA
Tuesday, 2022-11-29
My site
PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Site menu
Our poll
Rate my site
Total of answers: 3
Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
Main » 2012 » May » 22 » Pigo CCM uchaguzi 2015
1:38 AM
Pigo CCM uchaguzi 2015
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemaliza uchaguzi katika ngazi ya mashina na matawi huku kikikabiliwa na tatizo la kupata wagombea nafasi ya mabalozi wa nyumba kumi katika maeneo mbalimbali nchini.Uchunguzi wa gazeti hili katika mikoa mbalimbali, umebaini kuwa makada wengi wa CCM walikwepa kugombea nafasi hiyo jambo lililofanya walazimishane na kuleta wakati mgumu kupata warithi.

Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, mabalozi au wajumbe wa shina ndio ngazi ya kwanza ya uongozi ndani ya chama hicho pia ni kiungo muhimu kati ya chama na wananchi katika maeneo wanayoishi.

Mbali ya majukumu mengine, mabalozi wa nyumba kumi wamekuwa wahamasishaji wakuu wa chama katika maeneo yao, kuhakikisha wanachama wanajiandikisha kwenda kupiga kura pia kujua idadi yao kwenye eneo husika.

Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Augustino Mbogo, amekiri kuwa kazi ya kuchagua mabalozi wa nyumba kumi iliingia dosari na kufanya baadhi ya watu kususa.

Hata hivyo, aliwarushia lawama baadhi ya watendaji ndani ya chama hicho kwa ngazi ya Kata na Matawi kuwa walikuwa  kikwazo cha kukwamisha mchakato huo na kuwafanya baadhi ya wanachama  kususa.
Mbogo alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akielezea namna mchakato wa uchaguzi ndani ya chama unavyoendelea, ikiwemo uchaguzi wa ngazi ya mashina ambao umefikia kilele hivi karibuni.
Alisema kuwa katika wilaya yake, yako maeneo ambayo viongozi walitoa taarifa kuwa mabalozi walikuwa wakikataa kugombea na maeneo mengine waliamua kupeana nafasi hizo bila kufuata taratibu zozote.
"Ni kweli kuna baadhi ya maeneo hali haikuwa nzuri, mfano Kata za Chihanga,Hombolo na Mtumba tumepata wakati mgumu watu waligoma kugombea nafasi hizo,’’alisema Mbogo.
Kiongozi huyo alibainisha sababu za wanachama kugomea kugombea nafasi hizo ambapo alisema ni kutokana na ukiritimba mkubwa uliokuwa ukifanywa na baadhi ya makatibu wa maeneo husika.
"Unajua wale viongozi wa ngazi ya chini ni watu wa kuchaguliwa, hivyo katika maeneo mengi walikuwa wakipanga safu zao ili kujijenga na kuwa na mtaji wa wapiga kura pindi watakapoanza kugombea na wao,’’alisema.
Alitolea mfano kuwa baadhi ya maeneo fomu za kugombea nafasi hizo za mashina zilikuwa zikiuzwa kati ya Sh 5000 hadi 10,000 kinyume na utaratibu jambo lililofanya baadhi ya watu kushindwa kuzinunua.
Wakati Katibu huyo akieleza mchakato huo, uchunguzi uliofanywa katika baadhi ya maeneo umebainisha kuwa kwa baadhi ya sehemu, nafasi hizo hazikutangazwa kabisa,hivyo kufanya mabalozi waliokuwa madarakani waendelee kuongoza hata kama muda umepita.
Kata za Nzuguni, Iyumbu, Makutupora pamoja na maeneo ya Mpunguzi, Zuzu na maeneo kadhaa ya mjini Dodoma, uchaguzi huo haukufanyika na wengi hawajui kama mwaka huu ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi kwa mabalozi.
Kamati ya siasa Arusha yakutana

Uchaguzi wa Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa mashina, matawi na mabalozi katika wilaya tano za mkoa wa Arusha, umeelezwa kudorora  kwa kiasi kikubwa mwaka huu, huku wilaya za Arusha mjini na Arumeru zikishindwa  kabisa kufanya uchaguzi wa matawi.

Habari za uhakika kutoka ndani ya chama hicho, ambazo zimethibitishwa na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Mkoa wa Arusha, Loota Sanare, zimebainisha kuwa, kudorora kwa chaguzi hizo kumesababisha na sababu mbali mbali ikiwepo hali ya kisiasa mkoani Arusha.

Sababu nyingine zilizotajwa  na  baadhi ya viongozi wa CCM wa wilaya  mkoani hapa, ni pamoja na   kukosekana wagombea, na hivyo viongozi waliopo kuendelea kushikilia nafasi zao na kushindwa kusimamiwa zoezi la uchukuaji fomu, kurejeshwa na kupitisha majina kutokana na viongozi wengi kushiriki katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, uchaguzi wa matawi katika wilaya hasa za Arusha na Arumeru hadi jana ulikuwa haujafanyika, wakati uchaguzi wa mashina na mabalozi pia haujafanyika kwani wengi wa mabalozi, wameendelea na nafasi zao.

"Unajua mwaka huu, hapa Arusha tulikuwa na uchaguzi wa Arumeru kuanzia Januari hadi Aprili viongozi wengi walikuwa huko, hivyo ilishindikana uratibu wa chaguzi,"alisema kiongozi huyo.

Hata hivyo, alisema katika wilaya nyingine za Longido, Monduli, Karatu na Ngorongoro, uchaguzi wa ngazi za Mashina na matawi zimefanyika kwa wastani wa asilimia 80 tu.

Kutokana na hali hiyo, Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, ilitarajiwa kukutana jana kupokea taarifa za chaguzi hizo na kujua uhai wa chama katika wilaya zote.

Sanare alisema katika kikao hicho, kila wilaya itakuwa na ripoti yake ya chaguzi, hivyo kujulikana taarifa sahihi ni maeneo gani hazijafanyika na sababu zake, pia hatua ambazo zitachukuliwa.

"Naomba usubiri mara baada ya kikao cha Kamati ya Siasa tutakuwa na taarifa kamili ya chaguzi hizo na hali ya kisiasa ya mkoa wetu,"alisema Sanare.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa ambayo hali ya kisiasa imekuwa tete kwa CCM hasa kutokana na viongozi wake na makada kadhaa kujiengua na kujiunga na chadema.

Kinondoni

Akizungumza jana Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Aron Mwaikambo alisema chaguzi zilizo tayari ni za jumuiya pamoja na chama ngazi ya ubalozi na matawi.

Mwaikambo alisema, ubalozi wa nyumba kumi tangu Februari mwaka huu ila hapakuwa na upinzani kwa sababu sehemu nyingi ni mtu mmoja tu alijitokeza kugombea, hivyo kushinda bila upinzani.

 "Tulifanya uchaguzi wa nyumba kumi kuanzia Februari 2 hadi 5 mwaka huu tukamaliza zoezi hilo na tulipenda  kungekuwepo na upinzani ila watu walikua wachache na katika kila eneo la hizo nyumba kumi aliyechukua fomu ndio mshindi kwasababu  hapakua na upinzani kabisa”alisema Mwaikambo.Alieleza:

Sehemu nyingi wazee wamechoka hivyo wamewaachia vijana nafasi hiyo lakini asilimia kubwa ya vijana hawakujitokeza kwani licha ya balozi kuwa anatekeleza kazi za chama, pia ana jukuma la kupatanisha migogoro inayotokea katika nyumba hizo hasa familia ambapo kwa vijana inakua ngumu.

Temeke

Wakati hayo yakiendelea Kinondoni Msemaji wa CCM Wilaya ya Temeke, Saad Kusilawe amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimepata watu wengi waliojitokeza kuchukua fomu za ubalozi wa nyumba kumi katika kata zake zote.

Akizungumza jana ofisini kwake, alisema hali ilikuwa tofauti na alivyofikiria kwani waliojitokeza ni wengi tofauti na kipindi cha nyuma kulikuwa na wanachama wapatao 5,228 na katika kipindi hiki waliokuja kuchukuwa fomu hizo wamefikia 7,800 hali ambayo inaonyesha kuwa chama hicho bado kipo imara.

Kusilawe alisema hali ya siasa ina changamoto hasa kipindi hiki ambacho vijana wengi wamejikita katika suala la siasa  na kupelekea mambo kubadilika kutokana na kujitambua kwao.

"kwakweli vijana wamekuja juu sana kipindi hiki ila kinachoniogopesha ni kuhusu kuja kwao juu ni kwa kuchochewa na baadhi ya wanasiasa kufanya fujo na siyo kujenga nchi kama inavyofikiriwa”alisema kusilawe.

Aliongeza kuwa vijana wengi hivi sasa wamekaa kiushawishi na mara nyingi uacha mambo yanayowapeleka shule na kuanza kufanya siasa ambayo mara nyingi inakuwa ni hasara kwao kutokana na fujo wanazo zianzisha.
 
Dodoma
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma Mjini, Augustino Mbogo amekiri kuwa kazi ya kuchagua mabalozi wa nyumba kumi iliingia dosari na kufanya baadhi ya watu kususa.
Hata hivyo,  aliwarushia lawama baadhi ya watendaji ndani ya chama hicho kwa ngazi ya Kata na Matawi kuwa walikuwa ni kikwazo cha kukwamisha mchakato huo na kuwafanya baadhi ya watu kususia.

Mbogo alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akielezea namna mchakato wa uchaguzi ndani ya chama unavyoendelea ikiwemo uchaguzi wa ngazi ya mashina ambao umefikia kilele mwishoni mwa wiki.

Alisema kuwa katika wilaya yake yako maeneo ambayo viongozi walitoa taarifa kuwa mabalozi walikuwa wakikataa kugombea na maeneo mengine waliamua kupeana nafasi hizo bila kufuata taratibu zozote.

"Ni kweli kuna baadhi ya maeneo hali haikuwa nzuri, mfano Kata za Chihanga, Hombolo na Mtumba tumepata wakati mgumu watu waligoma kugombea nafasi hizo,’’alisema Mbogo.

Kiongozi huyo alibainisha sababu za wanachama kugomea kugombea nafasi hizo ambapo, alisema ni kutokana na ukiritimba mkubwa uliokuwa ukifanywa na baadhi ya makatibu wa maeneo husika.

"Unajua wale viongozi wa ngazi ya chini ni watu wa kuchaguliwa, hivyo katika maeneo mengi walikuwa wakipanga safu zao ili kujijenga na kuwa na mtaji wa wapiga kura pindi watakapoanza kugombea na wao,’’alisema.

Alitolea mfano kuwa baadhi ya maeneo fomu za kugombea nafasi hizo za mashina zilikuwa zikiuzwa kati ya Sh 5000 hadi 10,000 kinyume na utaratibu jambo lililofanya baadhi ya watu kushindwa kuzinunua.

Wakati Katibu huyo akieleza mchakato huo, uchunguzi uliofanywa katika baadhi ya maeneo umebainisha kuwa katika maeneo mengi nafasi hizo hazikutangazwa kabisa, hivyo kufanya mabalozi waliokuwa madarakani waendelee kuongoza hata kama muda umepita.

Hofu ya kutotangaza inatokana na ukweli kuwa baadhi ya mabalozi hawapendi kuendelea kuongoza na hivyo kama nafasi hizo zingetangazwa, ni wazi kuwa wangeweza kuziachia huku chama kikikosa mgombea katika eneo husika.
Kata za Nzuguni, Iyumbu, Makutupora pamoja na maeneo ya Mpunguzi,Zuzu na maeneo kadhaa ya mjini Dodoma, uchaguzi huo haukufanyika na wengi hawajui kama mwaka huu ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi kwa mabalozi.

Mara
Uchaguzi ngazi ya mashina na matawi ya  ya CCM umeshindwa kufanyika katika maeneo mbalimbali wilayani Serengeti ,kutokana na wanachama wengi kususa kujitokeza, hali iliyosababisha watu wateuliwe kushika ubalozi kinyume na utaratibu wa kawaida wa chama wa kupigiwa kura.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili ulibaini kuwa nafasi nyingi za ubalozi wa mashina  zimekimbiwa na wanachama wa CCM na sasa waliotayari wanateuliwa kujaza nafasi hizo.

"Hii ni aibu kubwa na haijawahi kutokea maana ilipofika kipindi hiki cha uchaguzi, watu walifukuzana kuwania ubalozi
,lakini leo mtu akionekana anachukua fomu ya ubalozi watu wanamzoea, hakika chama kinakwenda pabaya,”alisema Katibu mmoja wa Tawi la CCM, jina limehifadhiwa.

Katika Kata ya Manchira, mbali na uteuzi wa mabalozi na wengine kukataa uteuzi hata uchaguzi wa viongozi ngazi ya tawi uliokuwa ufanyike mwishoni mwa wiki hii ulishindikana baada ya wanachama wakiwemo waliochukua fomu, kutojitokeza.

Habari za uhakika na zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa matawi na Kata wa chama hicho, zinadai katika Tawi la Rwamchanga, walijitokeza watu wasiozidi wanane, hali iliyomlazimisha Katibu wa Uchumi wa Kata hiyo, John Wambura ambaye alikuwa msimamizi, kuahirisha hadi Mei 21 mwaka huu.

Hali hiyo pia iliyakumba matawi ya Ntamyo,Miserere na Miseke
ambapo wanachama hawakujitokeza hata waliojaza fomu za kuwania nafasi mbalimbali ,huku kukiwa na uvumi kuwa wana mpango wa kujiungua Chadema na wanasubiri viongozi wa kitaifa wahame.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Patrick Chandi alikiri kuwepo kwa migogoro baadhi ya maeneo ambapo amelazimika kumwagiza Katibu wake wa wilaya kufuatilia chanzo cha matatizo.

"Kwa ujumla tunaendelea ingawa kuna mambo hayawezi kwenda sawa sawa.
Maeneo kama Rwamchanga,Tamukeri ,Kisaka na kwingineko kuna migogoro ya ndani kwa ndani,”alisema.


Views: 14127 | Added by: twangaraha | Rating: 0.0/0
Total comments: 1
1 Shinyondo28v  
0
http://maxi-driver.pl/wynajmowanie-samochodow
Looking for a used or new auto might be a difficult procedure if you do not know what you are doing. By teaching yourself about car shopping before you decide to go to the dealer, you possibly can make issues much easier yourself. The following tips will help your next shopping vacation be a little more pleasant.

Usually deliver a auto mechanic alongside when looking for a whole new automobile. Vehicle dealers are well known for selling lemons and you do not desire to be their following sufferer. When you can not get yourself a auto mechanic to consider cars together with you, no less than make sure that you have him take a look at closing choice before buying it.

Know your boundaries. Before starting shopping for your car or vehicle, decide what you can manage to pay, and follow it. Don't forget to feature desire for your calculations. You will definitely pay out close to 20 % as a down payment also, so be ready.

Prior to going to a car dealership, know what kind of automobile you want. Research each one of you choices ahead of shopping so that you can figure out what works best for your financial allowance and family demands. Seek information to find out exactly how much you must pay for any probable vehicle.

Prior to signing any commitment spend some time to go through each and every range, like the fine print. If you have anything at all detailed you do not understand, usually do not signal before you get an response that you simply understand. Unsavory salesmen can make use of a binding agreement to place numerous fees that have been not talked about.

When you maintain the previous guidance in your mind when which you go looking for a car, you may be more prone to get a better offer. Purchasing a vehicle does not have to become frustration. Simply use the ideas with this write-up and you will obtain the auto you would like at a very good selling price.

Name *:
Email *:
Code *:
Login form
Calendar
«  May 2012  »
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031
NATHASON THE GREAT © 2022