PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Statistics |
Total online: 1 Guests: 1 Users: 0 |
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA
KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
|
Main » 2012 » May » 8 » Rufaa ya lema iko tayari
3:48 AM Rufaa ya lema iko tayari |
WAKILI Method Kimomogoro amekamilisha na
kuwasilisha mahakamani rufaa ya kupinga hukumu iliyomvua ubunge wa jimbo
la Arusha mjini, Godbless Lema huku akiainisha hoja 18 za kupinga
kukata rufaa. Kwa mujibu wa kumbukumbu za kimahakama zilizopatika
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, rufaa hiyo iliwasilishwa Ijumaa ya Mei 4,
mwaka huu tayari kwa ajili ya kuwasilishwa kwa msajili wa Mahakama ya
rufaa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusajiliwa.
Akizungumza
ofisini kwake jana, Wakili Kimomogoro alithibitisha kukamilisha na
kuwasilisha rufaa hiyo mahakamani tayari kwa ajili ya kupangiwa jopo la
majaji wa kuisikiliza.
Pamoja na hoja za rufaa, kitabu hicho cha
rufaa chenye kurasa 985 ina mwenendo mzima wa shauri, vielelezo na
viambatanisho vyote vilivyowasilishwa Mahakama Kuu.
"Kimsingi ni
rai yangu kuwa mtukufu Jaji Rwakibarila (Gabriel) hakutolea uamuzi mambo
na hoja za msingi zinazofanya hukumu yake kukosa hadhi kisheria, kuitwa
hukumu, hayo ni miongoni mwa hoja za msingi nilizoanisha kwenye rufaa
niyowasilisha mahakamani juzi,” alisema Wakili Kimomogoro.
Kwa
mujibu wa hati ya rufaa hiyo, hoja ya kwanza hadi nne zinapinga uamuzi
wa Jaji Aloyce Mjulizi aliyesikiliza shauri hilo katika hatua za awali
kwa kutupa pingamizi za awali zilizowasilishwa na upande wa utetezi
kwenye kesi ya madai namba 13 iliyofunguliwa na wapiga kura watatu
waliopinga ushindi wa Lema.
Miongoni mwahoja hizo ni kuwa wadai,
Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo hawakuwa na haki kisheria
kufungua shauri hilo kwa sababu hakuna haki yao iliyovunjwa kisheria
kama wapiga kura.
Wakili Kimomogoro aliyemwakilisha Lema na
mawakili wa Serikali, Timon Vitalis na Juma Masanja walidai aliyekuwa
mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian
ndiye alikuwa na haki kisheria kulalamikia ushindi na maneno ya kashfa yanayodaiwa kutolewa dhidi yake na Lema.
Hoja
ya tano hadi 18 zinapinga hukumu ya Jaji Rwakibarila ambapo katika
suala la hukumu yake kukosa hadhi kisheria, wakili Kimomogoro anadai
hakutolea maamuzi athari za wadai kushindwa kuwasilisha mahakamani CD
zinazomwonyesha Lema akitoa maneno ya kashfa na udhalilishaji walizodai
kuwa nazo katika hati yao ya madai.
Kimomogoro anadai Jaji
alikosea kwa kutotumia hata kesi moja kama rejea kati ya kesi kadhaa
zilizotajwa na mawakili wa pande zote mbili za wadai na wadaiwa.
Jaji
Rwakibarila ambaye ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga
pia anadaiwa kukosea kisheria kwa kukubali na kuegemea ushahidi wa mdomo
pekee katika hukumu yake bila kuwepo ushahidi wa mazingira, Video wala
maandishi kuunga mkono ushahidi wa mdomo.
Mrufani pia anadai Jaji
alikosea kwa kutumia viwango na vigezo tofauti kwa mashahidi wa upande
wa wadai na utetezi kwa kukataa ushahidi wa Leman na mashahidi wake kwa
madai kuwa walikuwa na maslahi kwa sababu ni wanachama na viongozi wa
Chadema lakini akakubali ushahidi wa wanachama na viongozi wa CCM
kutengua matokeo.
Hoja nyingine ni kuwa hata kama Lema angetiwa
hatiani kwa madai yaliwasilishwa mahakamani, bado Jaji hakustahili
kutumia kifungu cha 114 cha sheria za uchaguzi kuripoti uamuzi wake kwa
Mkurugenzi wa uchaguzi kwani makosa hayo hayahusiani na vitendo vya
rushwa wala jinai ambavyo humzua aliyehukumiwa kupiga kura wala kugombea
uongozi kwa miaka mitano.
|
Views: 596 |
Added by: twangaraha
| Rating: 0.0/0 |
|
|
|