PEEEEEOPLE'S POOOOOOOWEEEEEER NGUVU YA UMMAAA
Tuesday, 2022-11-29
My site
PAMOJA TUNAWEZA KULINDA TANZANIA
Site menu
Our poll
Rate my site
Total of answers: 3
Statistics

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0
JIUNGE NA CHADEMA UOKOE RASILIMALI ZA TAIFA KAMA RASILIMALI HAZITAANZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HUSIKA KATIKA TAIFA KUNA HAATARI YA TAIFA KUINGIA KWENYE VURUGU KAMA ILIVYO KUWA KWA SUDANI KUSINI
Main » 2012 » May » 11 » Sugu aelekea Ruvuma kuvuna wanachama
11:06 AM
Sugu aelekea Ruvuma kuvuna wanachama

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), leo anatarajiwa kuanza ziara ya kukijenga chama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kutoka Mbeya, Sugu alisema kuwa anaanza ziara ya kichama ya siku tatu mkoani Ruvuma, ambako atahutubia mikutano ya hadhara.

Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ alisema kuwa leo atafanya mkutano huko Madaba na kesho atakuwa mji mdogo wa Mbinga na Jumapili atamalizia mjini Songea.

"Leo nitaanza ziara ya siku tatu ya kichama mkoani Ruvuma, ambako nitaungana na viongozi wengine wa Chachema mkoani humo, kuhutubia mikutano ya hadhara ili kusaka wananchama wapya kutoka Nyanda za Juu Kusini,” alisema Sugu.

Katika hatua nyingine, Sugu alisema kuwa anashukuru kuona ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katikati ya mji wa Mbeya unaendelea vizuri, jambo linalompa faraja kwamba anatekeleza ahadi zake za kuwaletea maendeleo wakazi wa Mbeya.

Alisema kuwa anaamini ataweza kuzitimiza ahadi zake zote ndani ya muda muafaka kutokana na jinsi wananchi na watendaji wa Mbeya wanavyomuunga mkono.

"Kwa kweli ninafarijika kuona wananchi wa Mbeya pamoja na watendaji wa serikali wanaweka itikadi pembeni na wanakuwa na lugha moja katika kutekeleza miradi ya maendeleo,” alisisitiza Sugu.

Views: 2374 | Added by: twangaraha | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *:
Login form
Calendar
«  May 2012  »
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031
NATHASON THE GREAT © 2022