CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemaliza uchaguzi katika ngazi ya mashina na
matawi huku kikikabiliwa na tatizo la kupata wagombea nafasi ya
mabalozi wa nyumba kumi katika maeneo mbalimbali nchini.Uchunguzi wa
gazeti hili katika mikoa mbalimbali, umebaini kuwa makada wengi wa CCM
walikwepa kugombea nafasi hiyo jambo lililofanya walazimishane na kuleta
wakati mgumu kupata warithi.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, mabalozi au wajumbe wa shina ndio ngazi ya kwanza ya uongozi ndani ya chama hicho pia ni kiungo muhimu kati ya chama na wananchi katika maeneo wanayoishi. Mbali ya majukumu mengine, mabalozi wa nyumba kumi wamekuwa wahamasishaji wakuu wa chama katika maeneo yao, kuhakikisha wanachama wanajiandikisha kwenda kupiga kura pia kujua idadi yao kwenye eneo husika. Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Augustino Mbogo, amekiri kuwa kazi ya kuchagua mabalozi wa nyumba kumi iliingia dosari na kufanya baadhi ya watu kususa. Hata hivyo, aliwarushia lawama ... Read more » |
SAKATA la Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda kutangaza nia ya
kuwania urais ndani ya Kikao cha Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, sasa
linaitikisa Chadema baada ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la
chama hicho (Bavicha), Joliana Shonza kupingana hadharani na bosi wake,
John Heche.
Wakati Heche akiwa tayari ametoa tamko kumshambulia Shibuda akisema chama hicho hakitaruhusu mgombea wake urais atangaze nia kwenye vikao vya CCM, Shonza ameibuka na kusema tamko hilo la bosi wake siyo la Bavicha ila ni lake binafsi. Jana, Shonza akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, alilikana tamko la Heche wiki iliyoipita akisema hakuna kikao ambacho baraza hilo lilikaa na kutoa kauli moja kumjadili Shibuda. Hii ni mara ya tatu kwa Shibuda kusababisha mgongano ndani ya Chadema. Aliwahi kupinga msimamo wa kutotambua matokeo ya urais wa Jakaya Kikwete na badala yake, alishiriki tafrija Ikulu ndogo Chamwino, baada ya mkuu huyo wa nchi kuzindua Bunge la 10 n ... Read more » |
KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya
yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri
wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo
hao wanamiliki mali na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi.
Maofisa saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi. Tuhuma hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa kuanza kazi juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo itaanza rasmi kazi zake leo. Habari za uhakika kutoka ndani ya Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki akaunti ya fedha za kigeni. Kigogo huyo anahusishwa pia na mtan ... Read more » |
mwalimu nyerere ambaye ndiye mwasisi wa chama cha mapinduzi aliwahi kukitabilia kifo chama ambacho yeye aliki asisi kwa madai kua kina kanza ya uongozi hebu tupate nukuu ya maneno yake kabla htuja endelea
Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake: ... Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61) Mwalimu ... Read more » |
|
WANAHARAKATI nchini wamepinga mpango wa Ikulu wa kutaka kuwapo na
uchunguzi wa watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma
wanaotuhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma kwa kigezo kwamba
ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inatosha
kuwafikisha mahakamani.
Kauli hiyo imekuja baada ya juzi Ikulu kuagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwachunguza watendaji hao na kwamba uchunguzi huo kwa kile walichoeleza ni ili kutomuonea mtu wala kukandamiza wakati wa kuchukua hatua. Wakichangia maoni katika mada ya hali ya uwajibikaji nchini iliyotolewa kwenye Semina ya Maendeleo na Jinsia (GDSS), iliyofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam walisema , tuhuma zilizowaondoa kwenye nafasi zao ni za kushindwa kuwajibika na si za rushwa. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia katika mtandao huo, Diana Mwiru alisema ... Read more » |
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), leo anatarajiwa kuanza ziara ya kukijenga chama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kutoka Mbeya, Sugu alisema kuwa anaanza ziara ya kichama ya siku tatu mkoani Ruvuma, ambako atahutubia mikutano ya hadhara. Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ alisema kuwa leo atafanya mkutano huko Madaba na kesho atakuwa mji mdogo wa Mbinga na Jumapili atamalizia mjini Songea. "Leo nitaanza ziara ya siku tatu ya kichama mkoani Ruvuma, ambako nitaungana na viongozi wengine wa Chachema mkoani humo, kuhutubia mikutano ya hadhara ili kusaka wananchama wapya kutoka Nyanda za Juu Kusini,” alisema Sugu. Katika hatua nyingine, Sugu alisema kuwa anashukuru kuona ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katikati ya mji wa Mbeya unaendelea vizuri, jambo linalompa faraja kwamba anatekeleza ahadi zake za kuwaletea maendeleo wakazi wa Mbeya. Alisema ... Read more » |
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), amesema kuwa hana nia wala dhamira ya kuchochea na kuhamasisha mgawanyiko katika nchi kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu. Akizungumza na waandishi wa habari jana, juu ya maneno anayodaiwa kuyatoa Jumamosi kwenye mkutano wa hadhara wa chama chake wakati wa uzinduzi wa operesheni ‘vua gamba vaa gwanda’ kwenye viwanja vya NMC, Nassari alidai lengo la hotuba yake lilikuwa kuhimiza serikali na jeshi la polisi lishughulikie mauaji ya watu na kudai hakulenga kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake. "Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa; chama changu siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini wala historia, ningependa ifahamike kuwa sina lengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile kama ambavyo imekuwa ikita ... Read more » |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetishia kuweka hadharani majina ya mawaziri na wabunge ambao walikuwa tayari kujiunga na chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uenezaji wa chama hicho, John Mnyika, alisema Chama cha Mapinduzi kisitake kuilazimisha CHADEMA iseme ukweli wote juu ya wimbi kubwa la wana CCM, wakiwemo wabunge na mawaziri ambao wanataka kujiunga nayo. Mnyika akijibu taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, alisema kuwa viongozi wengi wa chama hicho tawala wanajua mchakato mzima uliokuwepo wa wabunge, mawaziri na wana CCM wengine kutaka kuhamia CHADEMA tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 lakini wakaingiliwa. Mnyika aliwataka viongozi wa CCM waseme kama wako tayari kupokea ukweli mchungu wa viongozi wao walio tayari kukihama chama hicho na kujiunga na upinzani "Wasitulazimishe kusema. Na kama wanataka waseme kama wak ... Read more » |
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko makubwa katika
Baraza lake la mawaziri, mawaziri na manaibu wapya wamesema
watahakikisha wanafanya kazi kwa maslahi ya Taifa na Watanzania.
Juzi Rais Kikwete alifanya uteuzi huo kwa kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza lake kwa kuingiza sura 13 mpya huku mawaziri na naibu mawaziri nane wakitupwa nje ya baraza hilo. Katika mabadiliko hayo, amewapandisha naibu mawaziri wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha mawaziri nane na naibu mawaziri sita, huku mawaziri na naibu mawaziri 22 wakibaki katika wizara zao za awali. Dk Mgimwa Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, alisema uteuzi huo ni jambo la heshima hivyo ni lazima kujituma na kufanya kazi kwa maslahi ya Watanzania. Alipoulizwa jinsi atakavyokabiliana na changamoto ndani ya wizara hiyo ikiwa ni pamoja na tuhuma zilizomng ‘oa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Mustapha M ... Read more » |